Sera ya Faragha
Michezo Leo · Ilisasishwa: 9 Oktoba 2026
Sera hii inaeleza jinsi app ya Michezo Leo (“app”) inavyotumia taarifa unapotafuta na kusoma habari, kutazama video, kuweka alama ya kupenda, kutuma maoni, au kuruhusu arifa. App inaendeshwa na timu ya Michezo Leo kupitia michezo.djmalogo.com.
Taarifa tunazokusanya
- Maoni: jina la kuonyesha na maandishi ya maoni unayotuma. Maoni yanaweza kukaguliwa; yakikubaliwa, jina na maoni yanaweza kuonekana kwa wasomaji wengine.
- Matumizi ya app: app hutuma kitambulisho cha kifaa cha Android pamoja na matukio ya views na likes ili kuhesabu matumizi na kusaidia kuzuia like kurudiwa. Taarifa hizi huhifadhiwa pamoja na rekodi husika za post. App haihitaji akaunti ya mtumiaji.
- Arifa: ukiruhusu arifa, Firebase Cloud Messaging hutoa tokeni ya kifaa. Tokeni huhifadhiwa kwenye server ili kutuma arifa za habari mpya.
- Matangazo: app hutumia Google Mobile Ads/AdMob na inaweza kutumia Meta Audience Network kupitia mediation. SDK hizi zinaweza kupokea kitambulisho cha matangazo, anwani ya IP, taarifa za kifaa/app, na mwingiliano na matangazo kwa ajili ya kuonyesha na kupima matangazo, kuzuia udanganyifu na kutatua hitilafu.
- Video: video za YouTube au huduma nyingine zinapofunguliwa, huduma husika inaweza kupokea taarifa za kiufundi kuhusu ombi la video na matumizi yake.
- Taarifa za kiufundi: server au watoa huduma wanaoweza kuhifadhi logi wanaweza kuchakata IP na taarifa za ombi kwa usalama, uendeshaji na utatuzi wa hitilafu.
Jinsi tunavyotumia taarifa
Tunatumia taarifa kutoa habari na video, kuhesabu views na likes, kusimamia maoni, kutuma arifa za post mpya, kuonyesha matangazo, kulinda huduma dhidi ya matumizi mabaya, na kurekebisha hitilafu.
Nani anaweza kupokea taarifa
Taarifa zinazohitajika kwa huduma zinaweza kuchakatwa na watoa huduma hawa: Google Firebase Cloud Messaging kwa arifa; Google Mobile Ads/AdMob na, pale mediation inapoitumia, Meta Audience Network kwa matangazo; na kampuni inayohost API na hifadhidata. Watoa huduma hawa huchakata taarifa kulingana na sera zao wenyewe. Hatupokei au kuhifadhi namba ya simu, mawasiliano, eneo sahihi, picha binafsi au taarifa za malipo kupitia app.
Uhifadhi na udhibiti wa taarifa
Maoni huhifadhiwa kwa ajili ya usimamizi na huenda yakaonekana hadharani yakikubaliwa. Rekodi za likes na views huhifadhiwa kwa takwimu za post. Tokeni ya arifa huhifadhiwa ili kutuma arifa, na inaweza kuzimwa au kuondolewa inapokuwa batili au baada ya ombi. Unaweza kuzima ruhusa ya arifa kupitia mipangilio ya Android.
Unaweza kuomba maoni yako au taarifa zinazoweza kutambua kifaa chako zifutwe kwa kuwasiliana nasi kupitia malogotito1@gmail.com. Huenda tukahitaji maelezo ya kutosha kutambua ombi na kulinda taarifa za watu wengine.
Usalama na muda wa kuhifadhi
Tunatumia HTTPS kwa mawasiliano ya app na server na tunachukua hatua za kawaida za kulinda hifadhidata na taarifa. Taarifa huhifadhiwa kwa muda unaohitajika kwa madhumuni yaliyoelezwa hapo juu, isipokuwa sheria au usalama wa huduma utahitaji muda tofauti. Hakuna njia ya kuhifadhi au kusafirisha data iliyo salama kwa asilimia 100.
Watoto
App ni ya habari za michezo kwa wasomaji wa jumla na haiombi taarifa nyeti kutoka kwa watoto. Mzazi au mlezi akiamini mtoto ametuma taarifa binafsi kwenye maoni, tafadhali tumia malogotito1@gmail.com kuomba hatua zinazofaa.
Mabadiliko na mawasiliano
Tunaweza kusasisha sera hii app au huduma zikibadilika. Tarehe ya toleo jipya itaonyeshwa juu ya ukurasa huu. Kwa maswali au maombi ya faragha, tumia malogotito1@gmail.com.
Privacy Policy
Michezo Leo · Last updated: 9 October 2026
This policy explains how the Michezo Leo app (“the app”) handles information when you browse sports news, watch videos, like posts, submit comments, or enable notifications. The app is operated by the Michezo Leo team through michezo.djmalogo.com.
Information we collect
- Comments: the display name and comment text you submit. Comments may be moderated; approved comments and display names may be visible to other readers.
- App use: the app sends an Android device identifier with view and like events to count activity and help prevent duplicate likes. These are stored with the related post activity. The app does not require a user account.
- Notifications: when you grant notification permission, Firebase Cloud Messaging provides a device token. The token is stored on our server to deliver new-post alerts.
- Advertising: the app uses Google Mobile Ads/AdMob and may use Meta Audience Network through mediation. These SDKs may receive an advertising identifier, IP address, app/device information, and ad interactions to serve and measure ads, prevent fraud, and diagnose issues.
- Videos: when YouTube or another provider’s video is opened, that provider may receive technical request and usage information.
- Technical information: our server or hosting providers may process IP addresses and request logs for security, operation, and troubleshooting.
How we use information
We use information to provide news and videos, count views and likes, moderate comments, deliver new-post notifications, serve ads, protect the service from abuse, and fix technical problems.
Sharing and service providers
Information needed to operate the app may be processed by Google Firebase Cloud Messaging for notifications; Google Mobile Ads/AdMob and, when mediation serves its ads, Meta Audience Network; and our API/database hosting provider. These providers process information under their own policies. The app does not request phone contacts, precise location, personal photos, or payment information.
Retention and your choices
Comments are retained for moderation and may remain visible if approved. Like and view records are retained for post statistics. Notification tokens are kept to deliver alerts and may be removed when invalid or upon request. You can turn off notification permission in Android settings.
You may request deletion of your comments or device-related information by contacting us at malogotito1@gmail.com. We may need sufficient details to identify the request and protect other people’s information.
Security and retention period
App-to-server communication uses HTTPS. We take reasonable steps to protect the database and information. Information is retained for as long as needed for the purposes above, unless a different period is required for legal or service-security reasons. No transmission or storage method is completely secure.
Children
The app provides sports news for a general audience and does not ask children for sensitive information. A parent or guardian who believes a child submitted personal information in a comment may request appropriate action at malogotito1@gmail.com.
Changes and contact
We may update this policy when the app or its services change. The latest revision date appears above. For privacy questions or requests, contact malogotito1@gmail.com.